Friday, 8 June 2018

Mama Lishe Mungu anawaona

Umakini unahitajika sana pale ambapo tunapata vyakula vyetu kwa mama/baba lishe. Kuna hatari ya kulishwa vitu ambavyo hatukuvitarajia; ikiwa ni pamoja na uchafu na sumusumu. kama huyu mama anavyotumia mifuko hii ya plastiki kufunikia ugali. Ni karibia mama lishe wote wanafanya hivi aidha kwa kujua au kutokujua. Tahadhari ndugu mlaji

Tuesday, 22 September 2015

Nguvu kazi ya Taifa

 Hii ni nguvu kazi ya Taifa. Nguvu kazi ambayo inatakiwa katika kuchangia kuleta maendeleo. Huyu atazunguka hivi kwa muda gani? Hata hivyo ni bora kuliko kufanya jambo ambalo linaashiria uhalifu.

Monday, 21 September 2015

Nguvu kazi ya Taifa

Nguvu kazi ya Taifa inayopotea kwa kufanya majikumu ambayo hayaendani na hali halisi. Kwa kijana kama huyu ilibidi awe anatumia nguvu zake kwa tija kuliko kuwa msafisha jiji kwa aina ya kipato akipatacho. Ni ajira sawa, ila haikupaswa kuwa katika mfumo huu. Wako wengi katika aina hii ya ajira inayokausha nguvu zao kwa kipato ambacho hakiendani na kazi wafanyayo. Hata hivyo ni bora kuliko kuwa mkabaji na kujiingiza katika aina nyingine yoyote ya uvunjifu wa sheria. 



Wednesday, 27 May 2015

It's like he is saying...

Thank you Father for this long awaited precious never forgettable wonderful day for this amazing woman before me. Lord you have heard my prayers. Lord you hear our prayers. Lord you listen to our inner voices begging for desires of our hearts. As I am smiling right now I believe that our hearts pound spontaneously to the rhythm of our breaths. Deep down between the middle of inner center to my heart I am humbled.  Lord spare us this life so we see our old age together. 

And somebody say, Amen...

Kamera inapokataa kutenda haki

Bi harusi 'akimnong'oneza' jambo bwana harusi baada ya kuvishana pete

Monday, 25 May 2015

Kipaimara

 Watoto wakijipanga kupiga picha ya pamoja na Baba Askofu Eusebius Nzigilwa baada ya Ibada ya Kipaimara katika kanisa la Kristo Mfalme Tabata siku ya Jumapili Tarehe 24/05/2015
 Baba Askofu akielekea kuzindua jengo la ofisi za mapadre katika kanisa hilo la Kristo Mfalme
Picha juu na chini Watoto wakiwa wamejipanga karibu na eneo zilipo ofisi mpya za Mapadre ambazo Baba Askofu Nzigilwa alizizindua hapo jana


Uharibifu katika ubunifu...

Au ni ubunifu katika uharibifu? Katika kuongeza ubunifu wa biashara na kukabiliana na ushindani ndio hutokea mambo kama haya. Wenyewe walikuwa hawajui ila walielezwa na kuonekana kuelewa. Sina hakika kama wataendelea na 'ubunifu' huu ama la maana ni kuua na kutokomeza uzalishaji wa maembe mengine zaidi.