Nguvu kazi ya Taifa inayopotea kwa kufanya majikumu ambayo hayaendani na hali halisi. Kwa kijana kama huyu ilibidi awe anatumia nguvu zake kwa tija kuliko kuwa msafisha jiji kwa aina ya kipato akipatacho. Ni ajira sawa, ila haikupaswa kuwa katika mfumo huu. Wako wengi katika aina hii ya ajira inayokausha nguvu zao kwa kipato ambacho hakiendani na kazi wafanyayo. Hata hivyo ni bora kuliko kuwa mkabaji na kujiingiza katika aina nyingine yoyote ya uvunjifu wa sheria.

No comments:
Post a Comment